MATOKEO ya awali ya uchaguzi
mkuu wa Angola yanaonesha kuwa chama tawala cha MPLA kimepata robo tatu
za kura - zimepungua kidogo kushinda uchaguzi uliopita.
Endapo idadi hiyo itathibitishwa matokeo yake ni
kuwa Rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi
ya miaka 30, atapata muhula mwengine wa uongozi.
Uchaguzi huo, wa tatu tangu Angola kupata uhuru mwaka wa 1975, ulikwenda vema ingawa awali kulikuwa na taarifa za ulalamishi.
Zamani Angola ilivurugwa na vita lakini katika miaka ya karibuni imepata utajiri wa mafuta.
0 comments:
Post a Comment