WATU wasiopungua 45 wameuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa
katika mapigano yaliyotokea kusini mwa kijiji cha Bibi kati ya majeshi
ya Kenya na Somalia kwa upande mmoja dhidi ya wapiganaji wa kundi la al
Shabaab.
Mapigano hayo yametajwa kuwa ndiyo makali zaidi kutokea huko kusini
mwa Somalia tangu majeshi ya Kenya yaingie nchini humo mwezi Oktoba
mwaka jana.
Mapigano baina ya pande hizo mbili yalishadidi zaidi baada ya jaribio
la majeshi ya Kenya na Somalia la kutaka kuingia katika ngome za kundi
la al Shabaab karibu na kijiji cha Bibi.
Hadi sasa hakujatolewa habari kamili kuhusu idadi kamili ya watu
waliouwa katika mapigano hayo kutoka pande zote mbili lakini vyombo vya
kuaminika vinasema makumi ya watu wameuawa.
Duru za kundi la al Shabaab zinasema kuwa ndege za kijeshi za Kenya zinashiriki katika mapigani hayo makali.
0 comments:
Post a Comment