MAWAZIRI wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) watajadili njia za kukabiliana na vitendo
vya dharau na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Balozi na mwakilishi wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa
Kiislamu (OIC) Hamid Reza Dahqani amesema kuwa mawaziri hao watajadili
njia za kukabiliana na dharau na vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu
ya Kiislamu katika mkutano wao wa 39 utakaofanyika nchini Djibouti na
ule utakaofanyika katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Ameashiria mikono ya nyuma ya pazia iliyohusika katika kuvunjia
heshima matukufu ya Kiislamu na kusema kuwa, Wamagharibi daima wamekuwa
wakidai kuwa masuala hayo yanatokana na uhuru wa kusema na kujieleza
katika katiba za nchi zao.
Dahqani ameongeza kuwa taasisi za kimataifa
zinasisitiza juu ya udharura wa kuheshimiwa dini za mbinguni, thamani na
itikadi za mataifa mbalimbali lakini inasikitisha kuwa hadi sasa juhudi
za jumuiya za kutetea haki za binadamu na jumuiya za kimataifa ikiwemo
OIC hazijafanikiwa kuwakinaisha Wamagharibi kuhusun ukweli kwamba uhuru
hauna maana ya kuvunjia heshima matukufu ya itikadi za watu wengine.
0 comments:
Post a Comment