CHAMA tawala cha Ukraine leo kimedai kushinda katika uchaguzi wa bunge
uliofanyika jana, huku matokeo ya awali yakionyesha kinakabiliwa na
ushindani kutoka kwa vyama pinzani vya Vitaly Klitschko na Yulia
Tymoshenko.
Waziri Mkuu wa Ukraine Mykola Azarov ameelezea uhakika wake kwamba chama
tawala kitashinda viti vingi katika bunge jipya baada ya uchaguzi wa
jana, ambao mataifa ya Magahribi yanaona ni mtihani mkubwa kwa
demokrasia ya Ukraine kutokana na kufungwa kwa mpinzani wa Rais Victor
Yanukovich.
Rais wa Ukraine Victor Yanukovich.
Hata hivyo chama cha bingwa wa masumbwi Vitaly Klitschko kinaonekana
kupoteza matarajio yake huku chama cha mchezaji soka Andriy Shevchenko
kikikuwa kinaonekana kushindwa vibaya katika uchaguzi huo.
Chama cha Rais Yanukovich kimepata asilimia 35.6 ya kura dhidi ya
asilimia 21.5 ilizopata chama cha upinzani cha Tymoshenko. Katika
taarifa yake, tume ya uchaguzi imezingatia asilimia 40 ya kura
zilizopigwa kwa mfumo sawa wa kuamua viti nusu vya bunge jipya.
Matokeo
ya awali yanaonyesha kuwa chama hicho tawala pia kilitarajiwa kushinda
angalau viti 110 kati ya 225 vya bunge.
Akielezea kuhusu uchaguzi huo
Azarov amesema wanategemea kuwa chama tawala kitapata viti vingi katika
bunge jipya.
Aidha, chama cha kikomunisti kilikuwa kimeshika nafasi ya
tatu kwa kupata asilimia 15.1ya kura na chama kipya cha UDAR
kilichojitenga na Klitschko kikiwa kimepata asilimia 12.8.
Urusi na Umoja wa Ulaya wanaufatilia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa jana ni mkubwa wa kwanza kufanyika nchini Ukraine ambao
umeonyesha mvutano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi tangu kiongozi
aliyefanya mapinduzi ya chungwa mwaka 2004, Tymoshenko kushindwa katika
uchaguzi wa urais mwanzoni mwa mwaka 2010, uchaguzi uliomuweka
madarakani Yanukovich.
Urusi inaufatilia uchaguzi huo kwa makini, huku
Umoja wa Ulaya ukitaka viwango vya demokrasia vizingatiwe, wakati ambao
Ukraine inaendelea kusisitiza nia yake ya kujiunga na umoja huo.
Waangalizi wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya-OSCE
wanatarajia kutoa maamuzi yao kuhusu uchaguzi huo baadae hii leo, ambayo
yanafatiliwa kwa karibu kabisa kuona iwapo kuna udanganyifu uliofanywa.
Viongozi wa Urusi na Umoja wa Ulaya.
Tymoshenko mwenye umri wa miaka 51, alikamatwa Agosti mwaka uliopita
wa 2011 na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana
na hatia ya kutumia vibaya madaraka, hukumu ambayo mataifa ya Magharibi
na wafuasi wake wanaona kama ni njama za kisiasa zinazofanywa
Yanukovich.
Wasiwasi kuhusu utawala wa miaka miwili wa Yanukovich
ulioigawa Ukraine kutoka kwenye mkondo wake wa demokrasia uliosababisha
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Mkuu wa sera za
kigeni wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton kutoa wito wa kufanyika
uchaguzi utakaozingatia demokrasia.

0 comments:
Post a Comment