Kimbunga Sandy kikiendelea kupiga majiji nchini Marekani baada ya kutoka Carribean na kupiga Canada.
KIMBUNGA kikali ambacho kimepiga nchini Marekani hasa upande wa Mashariki mwa
Taifa hilo kinachotambulika kwa jina la Sandy kimesababisha vifo vya
watu kumi na tatu huku melfu ya wananchi wakiendelea kuhama makazi yao
kujiepusha na madhara ambayo yanaweza yakajitokeza.
Madhara ya kimbunga
cha Sandy ambacho kinatajwa kutokea nchini Canada na kupiga maeneo ya
Pwani ya Marekani licha ya kusababisha vifo lakini kimewaacha watu zaidi
ya milioni tano na laki tano bila ya huduma ya nishati ya umeme
kutokana na miundombinu yake kuharibiwa.
Kimbunga cha Sandy kimeenda sambamba na kumiminika kwa theluji
kwenye maeneo mengi nchini Marekani kitu ambacho kimeongeza ugumu kwa
wananchi ambao wanahama makazi yao kupisha madhara ambayo yanaweza
kujitokeza kutokanana na kimbunga hicho.
Miundombinu ikiwa ile ya barabara imeharibiwa vibaya kutokana na maji
kujaa kwenye majiji mbalimbali nchini Marekani huku serikali wa
Washington ikiendelea kutoa tahadhari kwa wananchi kuondoka kwenye
maeneo ambayo yapo karibu na Pwani.
Kimbunga Sandy kabla hakijapiga nchi za Canadana na Marekani tayari
kilishasababisha vifo vya watu sitini na saba katika eneo la Carribbean
na hofu imeongezeka nchini Marekani idadi ya vifo inaweza ikaongezeka
kutokana na kutokea maporomoko.
Majiji ambayo yameathirika zaidi ya kimbunga cha Sandy ni pamoja na
New York, New Jersey, Pennsylvania, Maryland, West Virginia na North
Carolina ambapo Maofisa wameendelea kuwasihi wananchi kuondoka kwenye
makazi yao.
Kimbunga hiki kimeathiri kampeni za uchaguzi wa urais nchini Marekani
ambapo kwa mara ya pili Rais Barack Obama na hasimu wake Mitt Romney
wamelazimika kusitisha harakati zao za kunadi sera zao kupisha watu
kuondoka kwenye makazi yao.
Rais Obama naye ametumia fursa aliyoipata akiwa Washington kutoa wito
kwa wananchi kutii amri ambazo zinatolewa na Mamlaka husika kuhusiana
na taarifa za mwenendo wa kimbunga zinavyotolewa.
Shughuli nyingi zimetatizika ikiwemo kufungwa kwa shule na
kuahirishwa kwa safari za ndege na reli kutokana na kujiepusha na
madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na kuendelea kwa kimbunga cha
Sandy.
Kimbunga cha Sandy kimesababisha vinu vya nyuklia vilivyopo New
Jersey kuzingirwa na maji na tayari tahadhari imetolewa ya watu kukaa
mbali kwani kama ikivuja isije ikaleta athari.

0 comments:
Post a Comment