Iran itamaliza kiherehere cha Israel katika vita
NAIBU Mkuu wa vikosi vyote vya majeshi ya Iran Brigedia Jenerali
Masoud Jazayeri amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utajichimbia
kaburi lake wenyewe kwa kuanza kuishambulia Iran.
Brigedia Jenerali Jazayeri amesema utawala wa Kizayuni unaokalia kwa
mabavu Quds Tukufu sio tu hauna uwezo wa kuchuku hatua za kijeshi dhidi
ya Jamhuri ya Kiislamu, bali pia unafahamu vyema kwamba iwapo utaanza
kuishambulia Iran utakuwa unajichimbia kaburi lake wenyewe.
Naibu Mkuu wa vikosi vyote vya majeshi ya Iran amesema, makombora ya
Iran yanaweza kuzifikia kwa urahisi ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa
mabavu na Israel pamoja na maeneo mengine yenye maslahi ya Marekani
katika eneo la Mashariki ya Kati.
Inafaa kuashiria hapa kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel hivi
karibuni umezidisha vitisho vya kushambulia vituo vya nishati ya atomiki
vya Iran.
Vitisho hivyo vinatolewa kutokana na madai yasiyo na msingi
kwamba miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran inayoendeshwa kwa malengo ya amani eti lengo lake ni kutengeneza
silaha za nyuklia.
CHANZO// http://kiswahili.irib.ir.
0 comments:
Post a Comment