Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan na Kansela wa ujerumani Angela
Merkel wanakutana mjini Berlin huku suala kuu likiwa ni hali nchini
Syria. Uturuki inawahifadhi wakimbizi laki moja wa Syria.
Aliyesasema hayo wakati alipokutana na Waziri Erdogan mjini Berlin, ambaye leo anafanya mazungumzo na Kansela wa Merkel.
Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amezindua rasmi ubalozi wa nchi hiyo Ujerumani.
Wakati chama cha Westerwelle cha Free Democratic Party kikiunga mkono uwanachama wa Uturuki katika Umoja wa Ulaya, chama chake Kansela Angela Merkel cha Christian Democratic Union kinapinga.
Wakati Uturuki na Ujerumani zikiwa na uhusiano dhabiti wa kibiashara, uhusiano baina ya nchi hizo mbili wakati mwingine umeathirika kutokana na namna Ujerumani inavyowashughulikia wahamiaji kutoka Uturuki, pamoja na shutuma za Ujerumani kuhusu namna nchi hiyo inavyowashughulikia raia wake wa Kikurdi walio wachache.
Takriban watu milioni 2 na nusu wanaoishi Ujerumani wana asili ya Kituruki, na Erdogan amewaomba kuzungumza vyema Kijerumani pamoja na Kituruki, ili waweze kutangamana vyema katika taifa lao mwenyeji.
Jengo la ubalozi mpya wa Uturuki mjini Berlin, Ujerumani.
Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Erdogan kudokeza kuhusu muda ambao Uturuki huenda ikaendelea kuwa nao katika juhudi za kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Wakati huo Uturuki itakuwa ikiadhimisha miaka 100 ya uanzilishi wake kuwa Jamhuri kutoka kwa utawala wa Ufalme wa Ottoman.
Erdogan alisema Uturuki ambayo ina jumla ya idadi ya watu milioni 74 wengi wao Waislamu itauongezea nguvu Umoja wa Ulaya.
Takribani Waturuki milioni sita tayari wanaishi katika nchi za Umoja wa Ulaya, na takribani milioni tatu kati yao wanaishi Ujerumani.
Uturuki imekamilisha kifungu kimoja tu kati ya 35 vya sera ambavyo kila nchi inayotaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya lazima ikamilishe. Vifungu vyote vya sera isipokuwa 13 pekee katika mazungumzo ya Uturuki vinapingwa, na Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, ambayo ni mkono wa utendaji wa Umoja wa Ulaya, inasema Uturuki bado haitimizi viwango vinavyohitajika kuhusu haki za binaadamu na uhuru wa kujieleza.

0 comments:
Post a Comment