Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki akiwasalimia Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati alipofanya ziara ya kikazi leo katika Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki akionja chakula cha Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam alipotembelea sehemu ya jiko la Mahabusu na Wafungwa gerezani hapo .
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkaribisha Naibu wa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki (wa pili kushoto) azungumze na Maofisa wa Magereza katika ziara ya Kikazi aliyoifanya leo Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki akizungumza na Mahabusu na Wafungwa (hawapo pichani) wa Gereza la Keko jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo
0 comments:
Post a Comment