BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UCHAGUZI UVCCM MKOA WA IRINGA KUFANYIKA LEO.

 Mwanahabari na Mwanachama wa UVCCM Bi Tumain Msowoya ambaye ni mgombea nafasi ya kiti UVCCM mkoa wa Iringa.
 Mwanachama Gaudence Kabwabwalika anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa.
 Mwanachama Geofrey Lukuvi anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa wa Iringa.
Hawa ndio wagombea wa nafai ya UVCCM na ndio vijana wenyewe wa CCM


SAKATA la kashfa nzito kwa wana chama wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kutuhumiwa kudanganya umri wao wa kuzaliwa limechukua sura mpya baada ya idadi kubwa ya vijana waliojaza fomu za kuomba nafasi mbali mbali katika UVCCM kukimbia kikao cha usaili kwa wagombea hao.

Huku kamanda wa umoja wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emmanuel Mteming'ombe wakipigilia msumari kwa kutaka haki itendeke katika kuchuja majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali bila kuwepo upendeleo wowote na wale waliochakachua miaka kuwajibishwa .

Hatua hiyo imekuja baada ya mtandao huu kuibua siri nzito ya robo tatu ya vijana hao kujaza umri wa uongo ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma miaka ya kuzaliwa ili iweze kuendena na kanuni ya UVCCM inayomtaka mgombea kuanzia miaka 14-30.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu juzi wakati wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya UVCCM mkoa wa Iringa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa chini ya mgeni rasmi kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas.

Sehemu kubwa ya wanachama hao walioojaza fomu hizo kushindwa kutokea katika kikao hicho nyeti cha kuhakiki taarifa walizojaza katika fomu zao za kuomba nafasi mbali mbali.


Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wanachama zinadai kuwa walioshindwa kutokea katika kikao hicho ni baadhi ya wale wanaodaiwa kufanya uchakachuaji wa umri katika zoezi la ujazaji wa fomu hizo.
MWANAHABARI ABBA NGILANGWA APANIA MENGI UV CCM MKOA WA IRINGA.

Mwanahabari wa kituo cha Radio NuRu FM Iringa Abba Ngilangwa (pichani) ambaye ni mmoja kati ya vijana zaidi ya 10 wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa aliyejitosa kuwania nafasi hiyo amesema iwapo jina lake litapitishwa na kuwa mmoja kati ya wagombea wa nafasi hiyo ya kiti mkoa wa Iringa ana mengi ya kufanya.

Ngilangwa amesema kuwa kwa sasa ni mapema kuzungumza nini atafanya ndani ya UVCCM ila anazidi kumwomba Mungu pindi jina lake litakapopitishwa na kuwa mgombea na kushinda nafasi hiyo ataonyesha uwezo wake katika umoja huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: