BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Wanaharakati wa Mau Mau waruhusiwa kuishitaki Uingereza

 
 Muthoni Wanyeki, msemaji wa umoja wa wanaharakati wa Mau Mau akizungumza na waandishi wa habari.

BAADA ya madai hayo kukataliwa mwaka 2011, London baadaye ilidai kuwa muda mwingi ulipita kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki.
Mahakama moja nchini Uingereza imesema kwamba wazee watatu raia wa Kenya wanaweza kuendelea na mashtaka yao dhidi ya serikali ya uingereza   kwa shutuma za mateso wakati wa uasi wa wa mau mau enzi ya ukoloni.

Wakenya hao watatu  ambao hivi sasa wapo katika umri wa miaka ya 70 na 80  wanasema walipigwa na kunyanyaswa kingono na maafisa wa kikoloni wa Uingereza walipokuwa wakijaribu kukandamiza  uasi katika  miaka ya 1950.

London imejaribu kuzuia mashtaka hayo  ikisema jukumu la hatua kwa  shutuma hizo zilihamishiwa kwa serikali ya Kenya kufuatia uhuru mwaka 1963.

Baada ya madai hayo kukataliwa mwaka 2011, London baadae ilidai  kuwa muda mwingi ulipita kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: