BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AJALI ILIVYOKATISHA MAISHA YA SHARO MILIONEA MKOANI TANGA.


Alijitahidi, amejipatia usafiri maskini ya Mungu, kapata pa kulala, katoka Dar kwenda Tanga kuwaona wazazi kwa 
gharama zake mauti yamemkuta. Jambo la msingi 
tumuachie Mungu na kuondoa mawazo mabaya kuhusu na
 kifo chake.
GARI LIKIONEKANA BAADA YA AJALI HIYO.HUSSEIN RAMADHAN ‘Sharo Milionea’ (27) 
TASNIA ya sanaa ya hasa ya uigizaji, imekumbwa na giza lingine baada ya mmoja wa waigizaji mashuhuri, Hussein Ramadhani ‘Sharo Milionea’ (27) kufariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia jana.
Gari la mwigizaji hiyo lilipoteza mwelekeo na kupinduka mara kadhaa wakati akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda kijijini kwao, Lusanga mkoani Tanga, na kusababisha kifo chake saa 2.30 juzi usiku.
Mwandishi wa gazeti hili alifika nyumbani kwa wazazi wa msanii huyo jana na kupokewa na vilio vya waombolezaji.
“Masikini mdogo wangu, ametutoka akiwa mdogo, masikini mama yetu, ndoto za kujengewa nyumba na kuboreshewa maisha zimeishia barabarani,” ni maneno aliyokuwa akiyatoa dada wa marehemu.
Dada huyo aitwaye Rehema Kadiri (38) alilieleza Mwananchi kuwa msanii huyo alikuwa akienda kijijini, Lusanga kumpelekea mama yake mzazi fedha kwa ajili ya kulimia shamba.
Alisema ahadi hiyo alikuwa ameitoa wiki iliyopita alipokuwa amekwenda kijijini hapo kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu babu yake, Mkieta Juma aliyefariki dunia mwaka juzi.
Mazingira ya ajali
Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongiji cha Songa Kibaoni, Kijiji cha Songa, wilayani Muheza, Abdi Zawadi alisema ilipofika saa 2.30 usiku wakazi wa eneo hilo walisikia kishindo kikubwa ndipo wakaenda kushuhudia.
Alisema walipofika eneo la tukio, walikuta gari aina ya Harrier likiwa limepinduka, huku mwili wa mwanaume mmoja ukiwa pembeni, ndipo walipomfuata na kumkuta ameshakufa.
“Tulimtambua kuwa ni Sharomilionea baada ya kupekuwa mfukoni na kukuta kitambulisho cha mpiga kura kikiwa na jina la Hussein Ramadhani kikionyesha kuwa alijindikisha Lusanga, tukapaiga simu Kituo cha Polisi Muheza na askari wakaja kuuchukua mwili.
Mwananchi ilipofia eneo la tukio ilishuhudia mti mkubwa aina ya mjohoro uliogongwa baada ya gari hilo kuachia njia, ukiwa umeanguka na gari kupinduka hadi umbali wa mita kama 50.
Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema ndani ya gari hilo lalikuwamo dereva peke yake, likiendeshwa kwa mwendo mkali, na baada ya kupinduka dereva huyo ambaye ndiye msanii Sharomilionea alitupwa nje.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: