Hayati Yasser Arafat.
MWILI wa kiongozi wa zamani wa
Palestina, Yasser Arafat, umefukuliwa kutoka kaburi lake liloko ukingo
wa Magharibi mjini Rammala ili kuwawezesha kuufanyia uchunguzi kubaini
iwapo aliuwawa kwa sumu.
Arafat alifariki dunia mwaka 2004 nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.
Maradhi yaliyopelekea kifo chake hayakubainika.
Uamuzi wa kuufukua mwili wa Yasser Arafat katika kaburi lake lililoko
ukingo wa Magharibi unafuatia makala ya televisheni iliyodai kupata
mabaki ya madini ya kitonoradi aina ya Polonium kwenye nguo zake.
Wapalestina wengi wanashuku kwamba huenda Israel
ilihusika katika kifo cha kiongozi huyo.
Israel imekuwa ikikanusha
shutuma hizo.
Uchunguzi wa mauaji dhidi ya Arafat umeanzishwa nchini ufaransa kufuatia ombi lililowasilishwa na mjane wake.
0 comments:
Post a Comment