Kiongozi wa kijeshi wa kundi la M23 Brigadia-General Sultani
Makenga huko Goma.
WANAJEHSI WA VIKOSI VYA WAASISI M23 MJINI GOMA.
MKUU wa kisiasa wa kundi la M23 amesema majeshi yake yataondoka katika mji wa Goma mara moja kama serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo itatekeleza madai yao.
Jean Marie Runinga aliongea na waandishi wa habari Jumanne huko Goma mji ambao ulichukuliwa na waasi wiki iliyopita na baada ya hapo kuchukua mji wa Sake upande wa magharibi.
Mapema Jumanne , mkurugenzi wa mahusiano ya nje wa M23 Rene Abandi aliiambia VOA kwamba mkuu wa jeshi wa kundi hilo aliahidi majeshi yake yataondoka Goma haraka iwezekanavyo, baada ya mkutano na wakuu wa jeshi wa Uganda , Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Abandi alisema hatua hiyo haifanywi kwa shinikizo, ila ilikuwa ni dalili ya waasi kuridhia kufanya mazungumzo na serikali.
Wakati huo huo maafisa wa jeshi la Rwanda wanasema wahutu wenye msimamo mkali waliopo mashariki mwa Congo waliingia Rwanda Jumanne na kushambulia vijiji karibu na mpaka.
Msemaji wa jeshi alilaani majeshi ya waasi wa Rwanda (FDLR) kwa shambulizi hilo ambalo limepelekea mapigano na jeshi la Rwanda.
Shirika la habari la Reuters linaripoti Rwanda FDLR inayoipinga serikali ya Rwanda inayoongozwa na watusi imekataa kuwa inahusika na mapigano yeyote.
Rwanda imesema washambuliaji hao wanaofikia 100, walirudishwa nyuma na kurejea DRC au kwingineko nchini Rwanda.
Imesema wapiganaji 6 wa FDLR waliuwawa na wawili kukamatwa na raia mmoja aliuwawa
0 comments:
Post a Comment