
Ellinah Wamukoya.
Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo
katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata
siasaa za kihafidina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa la Kianglikana, likitarajiwa
kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa
hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika
Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na
pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia
sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyo,bo vya
habari, askofu huyo wa jimbo la Cape Town, Revd.
Thabo Makgoba, amesema
wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao
ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na
kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu
mweusi, muafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini.

0 comments:
Post a Comment