
David Beckham.
KLABU ya Paris Saint-Germain ni miongoni mwa vilabu maarufu duniani ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili David Beckham.
Beckham mwenye umri wa miaka 37, ametangaza kuwa
atakihama klabu ya Los Angeles Galaxy, baada ya kandarasi yake
kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.
Tayri
mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, amepokea ombi
kutoka kwa vilabu kadhaa nchini Urussi, Uchina, Australia na Brazil.
Ripoti zinasema, kuwa Beckham atakubali kandarasi na klabu yoyote ikiwa atatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wake 11 wa kwanza.
Beckham, anaripotiwa kutumia muda uliosalia
kabla ya kumalizika kwa mkataba wake kujadili uwezekano wa kusaini
mkataba na klabu nyingine.
Je Beckham atasajiliwa na klabu ipi?
Klabu ya PSG ilimpa Beckham kandarasi ya mamilioni ya paundi Novemba mwaka uliopita, lakini alikataa kusaini kandarasi hiyo kutokana na sababu za kifamilia.
Lakini baada y kuiongoza klabu ya LA Galaxy,
kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya pili nchini Marekani, Beckham
anahisi kuwa ni wakati muafaka kwake kuondoka.
Vilabu kadhaa nchini Brazil na Urussi
zimetangaza azma yao ya kutaka kumsajili Beckham, lakini habari ambazo
hazijathibitishwa zinasema kuwa mchezaji huyo kwa sasa anachunguza
uwezekana wa kucheza nchini Uchina.
Klabu moja kutoka Afrika Kusini pia imeonyesha
nia ya kumsajili mchezaji huyo, lakini huenda ikashindwa kutokana na
malipo ya mchezaji huyo.

0 comments:
Post a Comment