AIDAN LIBENANGA (68).
Bajeti katika nchi zilizoendelea ni lazima ilenge maendeleo ya watu na wala isilenge vitu au miundombinu ya barabara pekee yake lakini ilenge pia kwa wananchi ambapo itawapunguzia makali ya maisha, Bajeti sasa inalenga zaidi viongozi na Wabunge wa sasa wanapaswa kupitisha bajeti kulingana na hali ya maisha na hilo litasaidia wananchi waliowachagua watafaidika na ubunge wao bila kuzingatia itikadi zao za kisiasa.
HUU ulikuwa mchango wa mwandishi mkongwe Aidan Libenanga kwa upande wa Blog hii katika mahojiano yaliyofanyika mtaa wa Mlapakolo majira ya saa 6 mchana Jun 13 mwaka huu wakati akichangia BAJETI ya 2012/2013.
Aliyekuwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Morogoro, Queen Mwamshinga Mlozi, March 8/ 2009 ambaye kwa sasa ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Mwanza, akifafanua jambo kwa mwaandhishi mkongwe, Aidan Libenanga, kushoto juu ya hali ya elimu katika Manispaa hiyo wakati wa kikao cha watendaji wa elimu katika hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro.
UONGOZI MZIMA WA BLOG WWW.JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM UNATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU AIDAN LIBENANGA KWA KUFIKWA NA MSIBA HUO KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAJONZI,
MUNGU AILAZE MAHALA PEMA ROHO YA MPENDWA WETU PEPON AMIN.
KWA TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWALETEA KUPITIA BLOG HII.


0 comments:
Post a Comment