
DURU za habari kutoka Libya zinaripoti juu ya kuzimwa jaribio la
mapinduzi ya kijeshi yaliyopangwa na maafisa wa zamani wa jeshi la nchi
hiyo.
Taarifa zinasema kuwa, kundi la kwanza la maafisa hao tayari
limeshakamatwa katika mji wa Benghazi mashariki mwa nchi hiyo, huku
shirika la kijasusi la kijeshi la Libya likiendelea na msako wa kuwatia
mbaroni viongozi wengine wa mtandao huo huko Tripoli.
Hii ni mara ya
kwanza kutokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Libya tokea
alipong'olewa madarakani dikteta Kanali Muammar Gaddafi.
Hivi karibuni
kumetokea mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya viongozi
wa kisiasa na kijeshi nchini humo, miongoni mwao wakiwemo AbdulFattah
Younnis aliyekuwa Kamanda wa Operesheni za kijeshi dhidi ya vikosi vya
Gaddafi katika kipindi cha vita vilivyotokea mwaka uliopita nchini
humo, na Kanali Faraj al Darsi Kamanda wa Usalama wa Benghazi.

0 comments:
Post a Comment