SERIKALI ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo inasema haitazungumza na
wapiganaji wa M23 hadi waondoke mji wa Goma ambao waliuteka juma
lilopita.
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa
Maziwa Makuu mjini Kampala, Uganda, kuwasihi wapiganaji waondoke Goma.
Msemaji wa wapiganaji, Kasisi Jean-Marie Runiga,
alisema wapiganaji wataondoka Goma baada ya mazungumzo ya amani lakini
siyo kabla.
Rais Joseph Kabila wa Congo alikutana na wawakilishi wa wapiganaji mjini Kampala Jumamosi.
Wakuu wa Uganda wanasema yamekuwapo mawasiliano baina ya pande hizo mbili.

0 comments:
Post a Comment