Simba,
Nyati, Faru, Chatu haya ndiyo majina ya wanyama yanayoweza kukujia
akilini pindi ukiulizwa.
MNYAMA YUPI NI HATARI ZAIDI KWA MWANADAMU.
Well,
amini usiamini, kiumbe hatari zaidi ni mdogo mara elfu kadhaa
akilinganishwa kiumbo na hao majabali tunaowafahamu.
Na udogo wake si
katika umbile pekee bali pia hata sauti yake ni ndogo kulinganisha na
mbwa, paka au mbuzi, achilia mbali wababe kama Simba, Chui au Faru.
Kiumbe huyo hatari wa kuogopwa kwa gharama yoyote ile ni MBU.
Kwa mujibu wa takwimu, Mbu ni kiumbe hatari zaidi kuliko wote duniani. Kiumbe huyo hatari ni maarufu kwa kuambukiza rundo la magonjwa, kubwa zaidi ikiwa ni homa ya malaria.
Lakini pia mbu hueneza homa ya matende
(elephantiasis), homa ya manjano (yellow fever), kindiga popo (dengue
fever) na homa ya Mto Nile.
KESI DHIDI YAKE: Mbu anawajibika kusababisha kati ya vifo milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.
VIJIWE (Hangout) VYAO:
KESI DHIDI YAKE: Mbu anawajibika kusababisha kati ya vifo milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.
VIJIWE (Hangout) VYAO:
Takriban dunia nzima lakini zaidi barani Afrika, Asia na Amerika ya Kaskazini.
ANAVYOSABABISHA MAAFA:
ANAVYOSABABISHA MAAFA:
Mbu huambukiza maradhi ya kuuma kwenye ngozi ya
binadamu na kumwaga mate yake yenye vijidudu vinavyosababisha homa
husika.
Ukiweka kando vipele vidogo vinavyotokea mahala alipouma mbu,
anayeambukizwa na mbu hatambua maambukizo hadi pale kinga za mwili
inaposhtuka (na kuleta dalili mbalimbali).
JINSI YA KUMKWEPA:
JINSI YA KUMKWEPA:
Njia ya kupambana na mbu na maambukizo ni pamoja na
kutumia chandarua kilichomwagiwa kinga, kuangamiza sehemu za mazalio ya
mbu na vidonge vya kinga.
NYOKA WENYE SUKU KALI.
Japo kuna zaidi ya aina 2,000 za nyoka, 450 kati yao wenye sumu,ni aina 250 tu kati yao ndio wenye uwezo wa kuua binadamu.
KESI DHIDI YAO:
KESI DHIDI YAO:
Nyoka wenye sumu kali husababisha kati ya vifo 50,000 na 250,000 kwa mwaka.
VIJIWE VYAO:
VIJIWE VYAO:
Zaidi ni Afrika,Asia na Amerika ya Kaskazini
WANAVYOSABABISHA MAAFA:
WANAVYOSABABISHA MAAFA:
Nyoka wana kasi sana na sehemu yoyote katika
mwili wa binadamu inaweza kuwa kugongwa na kiumbe huyo hatari.
Lakini ni
hatari zaidi nyoka anapomgonga mtu kwenye mshipa wa damu kwani hiyo
huharakisha kusambaa kwa sumu ya kiumbe huyo.
Nyoka hutumia sumu yao
kumlegeza mtu na pengine kumpotezea fahamu.Majoka makubwa kama Mfalme
Kobra (King Cobra) yanaweza kusimama hadi usawa wa kichwa cha
binadamu,huku wengine wakiweza kutema na kurusha sumu yao kutoka mbali
kwenda kwenye macho ya mwanadamu.
JINSI YA KUWAKWEPA:
JINSI YA KUWAKWEPA:
Mara nyingi nyingi nyoka hushambulia pale tu pale
anapobughudhiwa.
Kwahiyo ushauri muhimu wa kuepuka shambulizi kutoka kwa
viumbe hao ni kujiepusha nao (Stay away!).
Pia ni muhimu kuvaa mabuti
kwenye mazingira yanayoweza kuwa na nyoka.Epuka mapori yanayoweza kuwa
makazi ya nyoka.
Na ikitokea umeomwona nyoka,inashauriwa urudi
kinyumenyume taratibu kwani anaweza kujirusha mara nusu ya urefu wake,na
mtikisiko kidogo tu unaweza kumasha hasira za kiumbe huyo hatari.
NGE.
Ni kiumbe hatari mwenye sura mbaya maradufu.Inaaminika kuwa ng'e anaweza kuwa anasababisha vifo vingi zaidi ya vile vinavyorekodiwa rasmi,sababu ya kuhisi hivyo ikiwa ni mazingira wanayoishi viumbe hao na ugumu wa kupatikana tiba dhidi ya sumu yao.
Hata hivyo,japo kuna aina tofauti 1500
za ng'e ni 25 tu kati yao ambao ni hatari kwa uhai wa uhai wa binadamu.
KESI DHIDI YAO:
KESI DHIDI YAO:
Ng'e husababisha kati ya vifo 800 hadi 2,00 kwa mwaka
VIJIWE VYAO:
VIJIWE VYAO:
Duniani kote hususan Afrika,America ya Kusini na Kaskazini na Asia ya Kati.
WANAVYOSABABISHA MAAFA:
WANAVYOSABABISHA MAAFA:
Ng'e humlegeza binadamu baada ya kumdunga sumu
kwa kutumia "vijisindano" vilivyopo kwenye mikia yao.
Kama ilivyo kwa
sumu nyingine za wadudu/wanyama,binadamu walio hatarini zaidi ni wale
wenye aleji,japo ng'e wengi wenye sumu wanaopatikana Afrika wanaweza
kumdhuru mtu yeyote yule.
JINSI YA KUWAKWEPA:
JINSI YA KUWAKWEPA:
Ng'e huwa active zaidi nyakati za usiku na
hupendelea kujipumzika mchana.Kwahiyo ni muhimu kuhakikisha sehemu ya
kujilaza ipo salama kabla ya kuubwaga mwili.
Kadhalika ni muhimu kupunga
mavazi na/au soksi kuhakikisha hakuna ng'e humo,vinginevyo itakuwa
balaa.
WENGINEO KWA KIFUPI
PAKA WAKUBWA (SIMBA, CHUI N:K)
Paka Wakubwa (kwa mfano yaani Simba,Chui,nk) husababisha takriban vifo 800 kwa mwaka
MAMBA.
Mamba husababisha kati ya vifo 600 na 800 kwa mwaka
TEMBO.
Pamoja na upole wao,Tembo husababisha kati ya vifo 300 na 500 kwa mwaka
KIBOKO
Mwamba huyo wa majini mwenye sura mbaya husababisha vifo kati ya 100 na 150 kwa mwaka.
KONYEZA (JELLYFISH).
Kiumbe huyu wa baharini husababisha takriban vifo 100 kwa mwaka.
PAPA.
Kiumbe huyu hatari wa baharini husababisha takriba vifo 100 kwa mwaka.
PANDA.
Husababisha kati ya vifo 5-10 kwa mwaka.
KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA http://www.kunambijr.blogspot.com











0 comments:
Post a Comment