![]() |
| Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera na uratibu wa bunge ,Wiliam Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani akimfariji msaidizi paroko wa Parokia ya Isimani Herman Myalla (36) wa Kanisa aliyelazwa Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuvamiwa na majambazi juzi. |
Picha na Habari na Francis Godwin.
RAIS Jakaya Kikwete amewafariji paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) waliojeruhiwa na majambazi huku akiziomba taasisi za dini kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yao kama njia ya kukomesha matukio ya ujambazi yanayofanyika katika maeneo ya taasisi za dini.
RAIS Jakaya Kikwete amewafariji paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) waliojeruhiwa na majambazi huku akiziomba taasisi za dini kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yao kama njia ya kukomesha matukio ya ujambazi yanayofanyika katika maeneo ya taasisi za dini.
Rais Kikwete alitoa wito huo kupitia waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani
mkoani Iringa ambako paroko huyo na mwenzake walivamiwa ,alitoa wito
huo leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa alipokuwa akiwasilisha
salamu za Rais Jakaya Kikwete na kutoa pole kwa Paroko Angelo Burgeo
(60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Isimani, wilayani Iringa.
Novemba 15, mwaka huu mapadri hao ambao wamelazwa katika hospitali ya
mkoa wa Iringa wakiendelea na matibabu, walivamia na kushambuliwa kwa
silaha za moto, mapanga na nondo na majambazi.
Watu watano wanaosikiliwa
na polisi wakihusishwa na uhalifu huo katika tukio hilo ambalo mapadri
hao mbali na kujeruhiwa vibaya waliibiwa zaidi ya sh Milioni
3.8.
Akiwasilisha salamu za Rais, Lukuvi alisema ametumwa kutoa pole kwa
wahanga hao, waumini na viongozi wa dhehebu hilo la dini kwa ujumla
wake.
“Tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ambacho majambazi wamekuwa
wakiwavamia viongozi wa dhehebu hili la dini wakiamini mmehifadhi fedha
na mali nyingine nyingi ndani ya parokia zenu,” alisema.
Alisema tukio la mapadri hao kuvamiwa na kujeruhiwa mkoani Iringa
limekuja miezi michache baada ya matukio kama hayo kutokea katika
parokia za Migori na Pawaga mkoani Iringa.
“Serikali imefanya kazi ya kutoa mafunzo kwa mgambo wengi karibu katika
kila kijiji, ni wajibu wa taasisi hizi za dini kuwatumia hao au
vinginevyo ikubali kushirikiana na jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa
walinzi wao,” alisema.
Akipokea salamu hizo, Padro Burgeo alisema majambazi hao walifanikiwa
kuingia ndani ya parokia yake baada ya kutumia lango la nyuma na
kufanikiwa kuwapiga chenga walinzi wao.
Alisema katika tukio hilo
ilikuwa afe lakini Mungu amesaidia kuyanusuru maisha yake baada ya
kufikishwa mikononi mwa madaktari.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Faustine Gwanchele alisema baada ya
kumfanyia upasuaji na kutoa risasi tatu kwa Padri Burgeo hali yake
inaendelea vizuri pamoja na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari



0 comments:
Post a Comment