Mkuu wa Jeshi la Polisi,IGP Said Mwema.
POLISI inaendelea na utaratibu wa ndani kubaini watendaji wake waliopo kwenye mtandao wa utapeli, kuhadaa watu kulipa kiwango fulani cha fedha ili watapatiwe ajira.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Msemaji wa Polisi, Advera Sonso inasema taratibu zimeanza kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo, kwani kilichofanyika ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za ajira jeshini.
Sonso katika taarifa hiyo anasema wanaamini mtuhumiwa wa kwanza ambaye amefikishwa mahakamani anayejulikana kwa jina moja la Komba, asingeweza kufanya utapeli huo pekee yake bila kushirikiana na watu wengine ndani na nje ya jeshi hilo.
“Tunaendelea na uchunguzi kwa kufuata taratibu za ndani, lengo ni kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Inawataka wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini mtandao huo.
Taarifa hiyo inabainisha kuwa mfumo wa ajira ndani polisi ni wa wazi na unafuata taratibu na kanuni zake, hivyo wananchi wanahimizwa kufuata taratibu na maelekezo yanayotolewa katika tangazo la ajira.
Polisi imewataka wote wenye malalamiko au taarifa kuwa walitoa fedha kupatiwa ajira na matapeli hao, au mawakala wao kutoa ushirikiano utakaowezesha polisi kukamilisha uchunguzi na hatimaye ushahidi kupatikana kusaidia kuthibitisha kesi mahakamani.
“Pia, taarifa zao zitatusaidia kuwapata wengine wote watakaothibitika kulingana na taarifa zitakazopatikana,” inasema taarifa hiyo.
Inawataka wananchi hao kutumia njia mbalimbali za mawasiliano au kufika Makao Makuu ya Polisi Kitengo cha Malalamiko.

0 comments:
Post a Comment