RAIS JAKAYA KIKWETE.
Jackson Odoyo na Happy Lazaro, Arusha
RAIS Kikwete amesema Serikali ilifanya makosa makubwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari kwa kushindwa kujenga maabara katika shule hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza sekta ya elimu ya Sayansi na Teknolojia nchini.

“Tulifanya makosa wakati tunajenga madarasa ile ya mikondo minne kwa sababu hatukukumbuka kujenga maabara mapema katika shule hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza elimu ya Sayansi na Teknolojia tangu awali.
Lakini hivi sasa Serikali imeliona hilo na ndiyo maana tukaamua kujenga Chuo Kikuu cha Utafiti wa Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichojengwa kwa fedha za Serikali,” alisema Rais Kikwete.
Chuo hicho mwaka jana kilidahili ya wanafunzi 83, huku wanafunzi 30 wakichukua masomo ya uzamivu na 53 ni mafunzo ya uzamili.
Mwaka huu kimedahili wanafunzi 135 wa kundi la pili, wakiwamo 46 wa masomo ya uzamivu na 89 wa uzamili huku asilimia 22 wakiwa wanawake.
Rais alisema kwamba wasomi watakaosoma katika chuo hicho ni wale wenye shahada ya kwanza baada ya kusoma katika vyuo vingine na watakapofika katika chuo hicho watakuwa na kazi ya kuzama zaidi katika elimu ya utafiti wa Sayansi na Teknolojia.
Rais Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi wa chuo hicho jijini Arusha, huku akifafanua kwamba Tanzania hivi sasa imeanza kuingia katika idadi ya nchi tajiri nakuondokana na umasikini kama Chuo hicho kitakuwa na maendeleo.

Katika hatua nyingine Rais Kikwete aliwataka wakuu wa chuo hicho,wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Profesa David Mwakyusa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Burton Mwamila kusimamia maendelea ya chuo hicho kwa dhati.
Naye Mkuu wa Chuo hicho, ambaye ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal akizungumnza alisema Serikali itajitahidi kukiboresha chuo hicho ili kiwe chachu ya maendelea barani Afrika.
Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete, alisema ili Nchi ya Tanzania iweze kukua katika viwango vya nchi ambazo
zinaendelea ulimwenguni ni lazima ihakikishe
kuwa kwanza inawekeza zaidi kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Katika hatua nyingine Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Burton Mwamila alisema kuwa, chuo hicho kitakuwa na faida kwa jamii.
”Tunategemea mabadiliko makubwa hasa kwa nchi ya Tanzania kwani chuo hiki kina uwezo mkubwa wa kuwapa fursa Watanzania kuwa na ujuzi wa kutosha hasa katika maswala ya tafiti na sayansi na kama Watanzania wataweza kukitumia vyema ni wazi kuwa fursa nyingi zitaongezeka sana”, alisema Profesa Mwamila.

0 comments:
Post a Comment