
WATU zaidi ya wanne wameuwawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya mkahawa mjini Mogadishu, Somalia.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kumetokea miripuko miwili mikubwa
nje ya mkahawa huo uitwao "The Village", katika mtaa wa Hodan,
kati-kati ya mji.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema mabomu yaliripuliwa na watu waliojitolea mhanga.
Mwezi wa Septemba watu 14 walikufa kwenye shambulio katika mkahawa mwengine mjini Mogadishu wa tajiri huyo-huyo.
Mwandishi wa BBC anakumbusha kuwa mashambulio
kama hayo hufanywa mara kwa mara, na baadhi yao ni vitendo vya kundi la
wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, ambao bado wanadhibiti sehemu kubwa
ya nchi.
Mashambulio mengine hufanywa na magengi ya wahalifu na wanamgambo.

0 comments:
Post a Comment