BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMANDA WA BOKO HARAM AUAWA NCHINI NIGERIA.

Silaha zilizonaswa na Jeshi
 Silaha zilizonaswa na Jeshi.

WANAJESHI wa Nigeria wanaendeleza operesheni kali ya kuwasaka wapiganaji wa Boko Haram katika eneo la Maiduguri Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Wanajeshi hao wanatumia magari ya kivita na wanapewa usaidizi zaidi na helicopta za kijeshi.

Jeshi la Nigeria limedai kuwa limemuua kamanda mmoja mwandamizi wa Boko Haram Ibn Saleh Ibrahim.
Raia wa eneo hilo wamesema kuwa idadi kubwa ya watu wameuawa kwenye operesheni hiyo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema Ibn Saleh Ibrahim aliuawa wakati wa makabiliano makali ya riasi wakati alipokuwa na walinzi wake sita.

Maafisa wa ulinzi nchini Nigeria wanaamini kuwa Saleh, alihusika na mauaji ya Generali mstaafu Mohammed Shuwa mwezi uliopita.

Kundi hilo la Boko Haram, ambao limeua raia wengi tangu mwaka wa 2009, halijasema lolote kuhusiana na kifo cha kamanda huyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: