
BARAZA la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma
Jumanne .
Azimio hilo limetoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja.
Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi wa Dw aliyekuwepo mjini New York
baraza hilo limepanga kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi hilo la M23
sambamba wanaowasaidia kutoka nje ya DRC.
Hata hivyo hawakufafanmua
zaidi kuhusu wasaidizi hao.
Aidha baraza hilo limemuomba katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
atoe mapendekezo yake kwa baraza hilo ya namna ya kufanikisha
kumalizika kwa mzozo katika eneo la Kivu.
Nguvu za kijeshi ziongezwe
Kikosi cha usalama cha Umoja wa Mataifa
Sambamba na hilo limesema kuna umuhimu wa kukiongezea nguvu zaidi
kikosi cha umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO ili kiweze kujihami
pamoja na kuwalinda raia.
Pamoja na mambo mengine katika mapendekezo yake kwa baraza la usalama
serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilitaka kuwepo kwa
aufafanuzi zaidi kuhusi kwa rwanda katika machafuko hayo ya mashariki
mwa Congo.
Rwanda yaendelea kujitetetea
Wakimbizi kutoka Goma
Kwa mujibu wa afisa mwandamzi wa Rwanda katika umoja wa Mataifa,
Olivier Nduguhungirehe aliendelea kukana kuhusika kwa taifa lake na
kundi la waasi wa M23.
Hata hivyo afisa huyoamesema kiniachoweza
kumaliza machafuko hayo ni mazungumzo kati ya waasi na serikali ya
Congo.
Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenyewe hali mjini Goma
inaelezwa kuwa mbaya zaidi huku idadi kubwa ya wananchi wakiwa katika
hofu ya usalama wao, wafungwa waliyoko magerezani wamefunguliwa.
Kupata
zaidi juu ya kile kinachoendelea, Sudi Mnette amezungumza na Mratibu wa
Jumuiya ya Kiraia, Mustafa Mwiti akiwa Goma.
Kusikiliza mahojiano hayo
bonyeza kitufe cha alama ya kusikiliza masikioni hapo nchini.

0 comments:
Post a Comment