BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUTANO MKUU WA 18 CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHINA CHAFUNGULIWA.


Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefunguliwa jana alasiri hapa Beijing. 

Rais Hu Jintao wa China leo ameshiriki kwenye majadilino na wajumbe kutoka mkoa wa Jiangsu na kudhihirisha kuwa, ripoti iliyotolewa jana kwenye mkutano huo ni taarifa ya kisiasa na mpango wa utekelezaji wa Chama cha Kikomunisti cha China kwa ajili ya kujipatia ushindi mpya katika ujenzi wa ujamaa wenye umaalum wa China. 

Amesema chama hicho kinapaswa kuchukua muda wa kujifunza na kutekeleza ripoti hiyo kama mwanzo mpya, kufahamu vizuri majukumu, kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii, ili kupata mafanikio makubwa zaidi.

Viongozi wengine wa China akiwemo spika wa bunge la umma la China Wu Bangguo, waziri mkuu Wen Jiabao na mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Jia Qinglin jana alasiri pia walishiriki kwenye mijadala ya wajumbe kutoka sehemu mbalimbali nchini China wanaohudhuria mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: