BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKURUGENZI MKUU BBC AJIUZURU KWA KURUHUSU KUPEPERUSHA KIPINDI KIMAKOSA

George Entwistle ajiuzulu kama Mkurugenzi BBC.

MKURUGENZI mkuu wa shirika la BBC, George Entwistle, amejiuzulu.


Amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.

Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto.

Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.

Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchnguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile.

Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya".

Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma".

"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika"
"Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amehiari kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika - uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi".
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: