BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA POLISI AUAWA BENGHAZI NCHINI LIBYA.

Wanajeshi wa Serikali ya Libya
Wanajeshi wa Serikali ya Libya.

 AFISA mmoja mkuu wa usalama nchini Libya amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake mjini Benghazi.

Wizara ya usalama wa ndani nchini humo imeelezea kuwa Bwana Farraj al-Dursi , ambaye alikuwa mkuu wa polisi mjini humo, amefariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Kumekuwa na visa vingi vya mauji mjini Benghazi katika siku za hivi punde.

Mnamo mwezi Septemba, balozi wa marekani mjini Benghazi aliuawa pamoja na wamarekani watatu katika ubalozi huo.

Col Dursia aliteuliwa kuwa mku wa polisi mjini humo muda mfupi baada ya shambulio lililotekelezwa kwenye ubalozi wa Marekani, ambalo balozi wa Marekani na maafisa watatu waliuawa.

Maafisa kadhaa wa Ulinzi wameuawa na watu wasiojulikana mjini Benghazi, mji ambao maandamano na machafuko yaliyomuondoa madarakani Muamarr Gaddafi yalianza.

Mwandishi wa BBC mjini Tripoli, anasema wengi wa maafisa hao wanalengwa kwa sababu wanakisiwa kuwa na uhusiano na serikali ya ya zamani ya nchi hiyo.

Kabla ya serikali, ya Gadaffi kuondolewa madarakani, Kanali, Dursi alifahamika kuwa afisa aliyehusika na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: