BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MANISPAA YA IRINGA YAKUMBWA NA HOFU YA MISUKULE.

 polisi  wakiwasaka  vijana  walioeneza uvumi wa kuwepo kwa msukule eneo la Mwangata mjini Iringa  sasa

 wananchi  wakiwa  wamesitisha  shughuli zao kutaka kuona msukule unaodaiwa kuonekana 
 Polisi  wakiwa katika msako wa kuwasaka wazushi wa taarifa  hiyo ya kuonekana mtoto anayedaiwa kufa  siku nyingi a.k.a Msukule
 Polisi  wakiwa katika msako eneo la Mwangata

Zimezuka  habari  zenye utata ambazo mtandao huu bado kuthibitisha  kuwa kuna mtoto anayedaiwa kufa na kuzikwa  kuonekana leo akidaiwa kuwekwa Msukule .

Tukio  hilo  limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa  na kupelekea  polisi  kufika  kuwatawanya  wananchi hao na kuwasaka  wale ambao wanadaiwa kueneza uvumi huo.

Hata  hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya  waliokuwepo hapo ambaye amethibitisha  kuona msukule  huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia .

Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka  kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule  huyo.

Rai ya mtandao  huu kwa jamii ya mkoa  wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuepuka kuamini  imani  za kishirikina ambazo zinaweza kuvuruga amani yetu
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: