PAKSTAN imemnyonga mwanajeshi aliyeshtakiwa kwa mauaji ya afisa wake mkuu baada ya rufaa ya mwanajeshi huyo kuomba msamaha kutupiliwa mbali.
Hii ni hukumu ya kwanza ya kunyongwa nchini humo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Pakistan imesitisha hukumu za kifo tangu Rais Asi Ali Zardari, alipochukua hatamu za uongozi mwa 2008.
Hata hivyo, makundi ya kutetea haki za Binadamu yamesema nchi hiyo ina idadi kubwa zaidi ya wafungwa waliohukumiwa kifo inayokisiwa kufikia elfu nane.

0 comments:
Post a Comment