Didier Drogba mmoja wa wanaowania tuzo za mchezaji bora Afrika.
Msenegali Demba Ba kushoto.
Alexandre Song wa Cameroon kushoto.
Msenegali Demba Ba kushoto.
Alexandre Song wa Cameroon kushoto.
Yaya Toure kushoto.
Andre
Ayew wa Ghana.
SHIRIKISHO la soka barani Africa CAF
limetangaza majina matano ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora
Afrika kwa mwaka 2012.
Didier Drogba wa Ivory Coast ambaye
aliisaidia timu yake ya zamani ya Chelsea kutwaa taji la Ligi ya
Mabingwa.
Drogba, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Shanghai Shenhua ya
nchini China.
Katika kinyang'anyiro hicho Drogba atachuana vikali na mtani wake Yaya Toure, wa Manchester City,
wanaungana na msenegali Demba Ba anayeichezea Newcastle United, Andre
Ayew wa Ghana na Alexandre Song wa Cameroon ambaye anakipiga na timu
Barcelona.
Watano hawa wamechaguliwa kutoka katika orodha ndefu ya wachezaji 10
kwa mujibu wa rais wa shirikisho la soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi,
ambaye pia ameshiriki katika bodi ya uteuzi ya CAF wakati akizungumza
na waandishi wa habari.
Hafla ya kumtaja mchezaji bora inayosimamiwa na CAF itafanyika Disemba 20 katika mji mkuu wa Ghana.


0 comments:
Post a Comment