Raia wakiwa wamejikusanya kwenye moja ya kifaru kilichotelekezwa na wanajeshi waliokimbia mji wa Goma.
UMOJA wa Mataifa umeelezea kushtushwa
na hali ya mambo Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
mara baada ya kushuhudia maelfu ya raia wakikimbia makazi yao kufuatia
kusonga mbele kwa waasi na kuteka miji kadhaa katika taifa hilo,na kutoa
wito wa msaada kwa wale walioathirika na ghasia.
DRC president Joseph Kabila.
Na katika kile kinachotajwa kuwa operesheni kubwa ya kwanza katika shughuli zake za kulinda amani, Umoja wa mataifa umesema kuwa unatazamia kutumia ndege zisizokuwa na marubani kufuatilia mapigano kati ya jeshi na waasi wa M23.
Viongozi wa ukanda wa maziwa makuu wanajielekeza jijini Kampala hii
leo kwa ajili ya mkutano kuhusu mgogoro wa karibuni huko Masharaiki mwa
DRC eneo lenye utajiri wa madini.

0 comments:
Post a Comment