Mwandishi mkongwe wa habari nchini aliyefariki dunia Nov 18 mwaka huu,
Aidan Libengana (64) akifafanua jambo moja ya mikutano ya chama cha
waandishi wa habari katika ukumbi wa New Savoy Hoteli hivi karibu mkoani
Morogoro.
Picha ya pamoja Aidan Libenanga wa kwanza kulia akiwa na wananchama na
viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro katika eneo
la hoteli ya New Savoy Morogoro, wa tano kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo
la Morogoro mjini Abdullaziz Abood.
MWANDISHI mwandamizi na ambaye amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na shirika la habari Tanzania (SHIHATA), Aidan Libenanga, anatarajia kuzikwa leo majira ya saa 10 jioni katika makaburi ya Kola Manispaa ya Morogoro.
MWANDISHI mwandamizi na ambaye amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na shirika la habari Tanzania (SHIHATA), Aidan Libenanga, anatarajia kuzikwa leo majira ya saa 10 jioni katika makaburi ya Kola Manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu huyo, Ramadhani Libenanga, marehemu alifariki dunia baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro majira ya saa 1.00 asubuhi juzi Nov 18/ 2012 akiwa anasubuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu (pressure).
Kuhusu wasifu wake Mzee Libenanga alizaliwa katika kijiji cha Libenanga tarafa ya Mwaya, wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na alipata elimu yake katika shule ya msingi Mwaya kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya wavulana ya Kwiro iliyoko mji wa Mahenge wilayani humo.
Baada ya kuhitimu elimu hiyo, Mzee Libenanga alichaguliwa kujiunga na sekondari ya Mzumbe kwa kidato cha tano na sita na hatimaye kuajiliwa kama mtumishi wa shirika la posta na simu nchini.
Mwaka 1975, mzee Libenanga alikuwa miongoni mwa waandishi wachache waliochaguwa na chama na serikali kwenda kusomea taaluma ya uandishi wa habari ambapo alikwenda nchini Yugoslavia na kufaulu kwa ngazi astashahada (certificate) na stashahada (diploma) ya uandishi wa habari.
Marehemu aliajiriwa na serikali katika shirika la habari Tanzania kama mkuu wa habari (Bureau chief) katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Iringa, Kigoma, Shinyanga, Rukwa na Morogoro na baada ya kustaafu kazi alibaki kuwa mwandishi wa kujutegemea akifanya kazi na vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti.
“Baba huwa anapenda kufua nguo zake mwenyewe, sasa na asubuhi hiyo aliamka kufua nguo hizo lakini alipoingia bafuni ghafla alidondoka na tukampeleka hospitali ya mkoa kwa matibabu,” alisema Libenanga.
Alisema kuwa cha kusikitisha sana baada ya kufika hospitalini hapo huduma za matibabu kwa baba yake zilichelewa kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wa ajali ya barabarani waliofikishwa hospitalini hapo muda huo na hivyo kusababusha mwandishi huyo mkongwe kupoteza maisha akiwa katika harakati za kupatiwa matibabu.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu, Aidan Libenanga, Amina.




0 comments:
Post a Comment