BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DKT KIKWETE AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MAKWETA.

Rais Jakaya Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo ya marehemu Jackson Makwetta alipokwenda kutoa heshima ya mwisho na kuuaga mwili nyumbani kwa marehemu, Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, jana. Picha na Ikulu.


DKT Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe, Jackson Makwetta.  

Mwili wa marehemu Makwetta utasafirishwa kwa ndege leo saa 3:00 asubuhi kuelekea kijijini kwake Njombe, baada ya kuwasili wananchi watapewa fursa ya kuuaga tena.

Wakati wa kuuaga mwili huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliitaka serikali kuchunguza miradi na mali za viongozi kulingana na kipato walichonacho.Alisema mali alizonazo Makwetta ni ndogo ukilinganisha na muda aliyokaa madarakani.


Mbowe alisema baadhi ya viongozi walioko madarakani hivi sasa, wana mali nyingi kuliko kipato chao jambo ambalo linaonyesha wazi ni mafisadi.

“Makwetta anaonyesha wazi kuwa siyo fisadi ikilinganishwa na mali alizokuwanazo, wakati baadhi ya viongozi wa sasa wana mali nyingi kuliko vipato vyao,” alisema Mbowe.


Alisema Makwetta amefanya kazi kwa miaka 35, lakini mali alizonazo ni ndogo, hivyo viongozi wa sasa wanapaswa kuiga mfano huo.

Naye Spika wa Bunge, Anna Makinda alisema marehemu Makweta aliwahi kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, pia alianzisha Mfuko wa Maendeleo Njombe ambao haujazinduliwa.
“Makwetta aliandaa mpango mkakati wa maendeleo wa Wananjombe ambao haujazinduliwa,” alisema Makinda.

Kwa upande wa Serikali mazishi hayo yataongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Uratibu na Sera), William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Siasa), Stephen Wassira na CCM itawakilishwa na Makamu mwenyekiti wake, Phillipo Mangula.

Marehemu Makwetta alifariki Jumamosi iliyopita kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali Kuu ya Kijeshi Lugalo. 


Anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake, mkoani  Njombe.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: