Waasi wa M23 wamewalazimisha watu kutoroka mji wa Goma.
KIONGOZI wa waasi wa M23 ambao wiki
iliyopita waliuteka mji wa Goma Mashariki mwa DRC, wanasema katu
hawataondoka Goma hadi serikali itakapotimiza matakwa yao.
Kiongozi wa kundi hilo, Jean-Marie Runiga
alisema kuwa wapiganaji wake wataondoka mara moja ikiwa Rais Joseph
Kabila, ataitikia matakwa yao ambayo ni pamoja na kuivunja tume ya
uchaguzi.
Serikali ya Congo hata hivyo imepuuza matakwa hayo kama ya kipuuzi.
Uganda ambayo imekuwa ikipatanisha pande hizo
mbili kwenye mkutano mjini Kampala, awali ilisema walikubali kuondoka
Goma bila vikwazo.
Mnamo Jumamosi, serikali za nchi za Maziwa makuu ziliwapatia waasi hao makataa ya siku mbili kuondoka Goma.
0 comments:
Post a Comment