
Vifaru wanakabiliwa na tisho la kuwindwa kiharamu.
MAHAKAMA nchini Afrika Kusini imemhukumu
kifungo cha miaka arobaini raia mmoja wa Thailand aliyepatikana na hatia
ya kuuza pembe za vifaru na kuandaa maonyesho ya uwindaji
yasiyokubalika.
Chumlong Lemtongthai alikiri kosa la kuwalipa makahaba kuweza kufanya maonyesho ya uwindaji wa vifaru.
Pembe hizo ziliuzwa barani Asia ambako soko la pembe hizi ni kubwa sana kwani hutumiwa kama dawa.
Zaidi ya vifaru miatano wameuawa nchini humo na wawindaji haramu mwaka huu pekee.
Akitoa hukumu hiyo jaji alisema kuwa hataki wajukuu wake wakuwe bila kujionea vifaru nchii humo.

0 comments:
Post a Comment