
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema visa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria vimeongezeka kutokana na mafuriko hayo, ingawa hakuna mlipuko mkubwa ulioripotiwa. WHO pia imeeleza uharibifu uliofanyika dhidi ya majengo na vifaa vya afya katika maeneo yaloathirika.
Nalo Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema maeneo yaloathirika hayana huduma za maji safi, kwani asilimia 63 ya maji ya kunywa na kupikia hutoka kwenye mito na visima vilivyo wazi.
Afisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA limesema ingawa mafuriko hayo yanapungua, mashirika ya kibinadamu yanakadiria kuwa gharama ya mahitaji ya kibinadamu ni dola milioni 38, hasa katika majimbo 14 yaliyoathirika zaidi. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

0 comments:
Post a Comment