
Watu wakikimbia mapigano ya waasi katika mji wa Goma nchini Congo mji huo una utajiri mkubwa wa madini.
Msimamo huo wa Serikali umetolewa huku juhudi za
kutafuta namna ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo zikiendelea mjini
Kampala, Uganda, ambapo viongozi wa nchi zinazopakana na DRC wakikutana
kutafuta msimamo wa pamoja.
Kauli hiyo ya Membe imetolewa wakati wapiganaji wa
M23 wanaoipinga Serikali ya Kongo wakisisitiza kwamba sasa hivi
wanajipanga kupambana kuelekea Bukavu, Kisangani kisha mji mkuu wa nchi
hiyo, Kinshasa.
Pia, imeitaka UN kutoa kibali cha kuyaruhusu
majeshi ya umoja huo yanayolinda amani nchini Kongo kupambana waasi hao
wa M23 ili kuweza kuwang’oa na kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Sisi nchi za SADC na maziwa makuu tukiruhusiwa
tukienda tuna uwezo wa kupambana na kuwaondoa hao M23 wanaosumbua lakini
tunachohitaji ni ruhusa kutoka UN kwani wanajeshi wanaohitajika
kufanikisha hilo ni 4,000,” alisema Membe na kuongeza;
“Hivi sasa majesi ya UN yaliyopo Kongo yanafanya
kazi chini ya kibali namba sita cha UN ambacho kinawataka wao kulinda
amani tu, tunaomba katibu mkuu wa umoja huo atoe kibali namba saba ili
majeshi hayo yapambane na waasi wa M23 na kuwaondoa.”
Membe alisema kuwa hivi sasa Serikali
inasikitishwa kwa kushindwa kwa majeshi ya UN kuwazuia waasi wa M23
wasiteke mji wa Goma kwani kitendo hicho kinawapa nguvu waasi kuendelea
na mapambano.
“Tunawataka waasi wote waiachie Goma kwa kuwa
kilichotokea hakikubaliki, tunasikitika vikosi vya UN kushindwa kuzuia
hilo, tunamuomba katibu mkuu wa UN atoe kibali kuruhusu wanajeshi wake
wapambane ili kuzuia waasi wasiendelee na vita,” alisema Membe na
kuongeza;
“Hatukubaliani na utekaji huo na kwamba kama wakiendelea na kuiteka Bukavu, tutapata wakimbizi wengi kutoka Kongo.”
Alisema wakati Serikali ya Tanzania ikitoa tamko
lake kuhusu waasi hao leo viongozi wa nchi za maziwa makuu watakutana
nchini Uganda na kufanya mazungumzo ambayo yatatoa uamuzi mgumu kama UN
haitaruhusu majeshi yake au ya maziwa makuu kuingilia kati vita hivyo.
“Kesho (leo) na keshokutwa (kesho) uamuzi mgumu
utatolewa ambao utalitatua tatizo la Kongo moja kwa moja,” alisema
Waziri Membe na kuongeza;
“Tunailaumu UN kwa kutokuchukua maamuzi hayo magumu ya kuweza kuzuia vita nchini Kongo.”
“Tunailaumu UN kwa kutokuchukua maamuzi hayo magumu ya kuweza kuzuia vita nchini Kongo.”

0 comments:
Post a Comment