BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI WAANZA RASMI LEO WA KUCHAGUA RAIS WA NCHINI.

Wagombea Barack Obama na Mit Romney.

RAIS Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu ya White House.


Mwandishi wa BBC ambaye yuko kwenye kampeini ya Romney, anasema kuwa hizi dakika za mwisho ni kuhusu kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi huu wenye ushindani mkali.

Kura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. 

Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: