BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Wafanyabiashara magendo wajaribu kumuua mwanahabari


WAFANYABIASHARA wanaosafirisha sukari kwa magendo kwenda nchini Kenya, juzi walifanya jaribio la kumuua mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima mkoani Kilimanjaro, Charles Ndagulla.
Tukio hilo lilitokea saa 6:00 usiku, baada ya wafanyabiashara hao wakiwa na gari aina ya Toyota RAV 4J, kumgonga kwa makusudi mwandishi huyo na kufanikiwa kuvusha malori mawili yakiwa na sukari.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ambalo limeibua maswali mengi, kuhusu kiburi cha wafanyabiashara hao hadi wafikie hatua ya kutaka kutoa uhai wa mwandishi ili kutimiza malengo yao.
Kabla ya waandishi wa habari za uchunguzi kwenda eneo la Holili karibu na machimbo ya madini ya Pozorana, walidokezwa kuwa malori 12 aina ya Fusso yangevuka mpaka usiku kwenda Kenya.
Malori hayo yalikuwa yaanzie safari zake mji wa Himo na kuelekea barabara ya Himo-Holili, kisha yangechepuka na kushika barabara ya Lower Rombo hadi eneo hilo la madini na kuingia Kenya.
Mpaka waandishi wa habari wanafika eneo ulipotokea mkasa huo, tayari malori sita yalikuwa yameshavuka mpaka kupitia njia za panya eneo la Holili kati ya saa 4:00 na saa 5:00 usiku huo.
Lakini, kabla ya waandishi wa habari kwenda eneo hilo, walimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz ambaye aliahidi kuwaandaa polisi kwa lengo la kukamata malori hayo.
Baada ya kufika eneo hilo, malori hayo yalijitokeza na waandishi waliyasimamisha na madereva wake kutii amri hiyo, Mwandishi wa habari hizi alimtaarifu Kamanda Boaz muda huohuo.
Pia, mwandishi wa habari hizi alimtaarifu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Patience Minga ambaye aliahidi kutuma maofisa wake wa doria.
Lakini wakati waandishi wakisubiri msaada wa polisi, ilifika gari ndogo aina ya RAV 4J ikiwa na watu wawili mmoja mwanamke, ambao waliwaamuru madereva hao kuondoa kwa nguvu malori hayo.
Mwandishi wa Tanzania Daima ambaye alikuwa upande wa yalipokuwa yakielekea malori hayo, aliwamulika kwa tochi watu waliokuwa katika gari ndogo ndipo walipomfuata na kumgonga.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: