
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO)
limesema zaidi ya humusi moja (1/5) ya vijana nchini Tanzania hawamalizi
elimu ya msingi na hawana ujuzi wa kufanya kazi.
Taarifa hiyo imetolewa
wakati wa uzinduzi wa 10 wa Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote
jijini Dar es Salaam.
UNESCO imeeleza kuwa zaidi ya vijana milioni 56
wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 walioko Chini ya Jangwa la Sahara
hawakumaliza elimu ya msingi wala hawana ujuzi wa kufanya kazi. Pia
katika dunia nzima thumni moja (1/8) ya vijana hawana ajira.
Kufuatia
ripoti hiyo ya UNESCO, Kamishina wa Elimu katika Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi ya Tanzania, Profesa Eustell Bhalalusesa amesema
wizara hiyo inafanya mapitio ya sera ya elimu ili kuhakikisha sekta hiyo
inaimarika.

0 comments:
Post a Comment