BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKOFU ATAKA WACHEZA KAMARI WATOE SADAKA.

Rowan Williams ambaye anastaafu mwaka ujao
ASKAOFU Justin Welby, aliyeteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, yaani Askofu wa Canterbury, amependekeza kwenye mtandao wa Twitter kwamba mtu yeyote aliyeshinda kwenye kamari kwa kubahatisha kuwa yeye ndiye atateuliwa, anafaa kutoa fedha hizo kama sadaka kwa kanisa.

 Mwanzo wa juma hili makampuni ya kamari yalitangaza kuwa yamesimamisha kamari juu ya nani atakuwa kiongozi mpya wa kanisa la Anglikana, kwa sababu wengi walifikiri kuwa ni Askofu Welby, ambayo inaonesha baadhi ya maafisa wakijua kuwa jina hilo ndilo lilopendekezwa.

Askofu Welby atachukua nafasi ya Rowan Williams mwaka ujao kuwa kiongozi wa wamumini wa Kianglikana dunia nzima.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: