STAKABADHI za Serikali zilizotolewa huko
Uingereza zinaonyesha kwa ukamilifu namna wafungwa wengi waliuawa wakati
wa uasi wa kundi la Mau Mau nchini Kenya.
Wakenya kumi na mmoja walipigwa na walinzi hadi kufa katika kambi walikozuiliwa ya Hola huku wengine wakijeruhiwa mwaka 1959.
Baadhi ya wapiganaji wa Mau Mau waliodhulumiwa na wakoloni wa Uingereza.
Mzee moja manusura wa mauaji hayo kwa sasa ameshtaki serikali ya Uingereza akidai aliteswa.
Stakabadhi hizo zinaonyesha mkutano uliongozwa
na aliyekuwa gavana wa Kenya na maafisa wakuu wa magereza kumbukumbu
zinazoonyesha kuwa maafisa hao walikiuka haki za binadamu lakini
hawakufunguliwa mashtaka.
0 comments:
Post a Comment