MAMIA kwa maelfu ya waandamanaji waliingia mitaani mjini Cairo jana
Ijumaa kuongeza mbinyo kwa rais Morsi baada ya jopo lenye
wajumbe wengi kutoka kundi la Kiislamu kupitisha mswada wa katiba wa
nchi hiyo.
Katiba hiyo mpya , ambayo imeidhinishwa baada ya vikao virefu usiku wa
jana na ambayo imesusiwa na wajumbe wenye msimamo wa kati na Wakristo,
inazua wasi wasi mkubwa kuhusu masuala ya haki za binadamu, ikiwa ni
pamoja na uhuru wa kidini, wanasema wanaharakati.
Morsi atapitia upya mswada huo leo Jumamosi,(01.12.2012), amesema spika
wa bunge Hossam el-Ghiriani, na anatarajiwa baadaye kuitisha kura ya
maoni katika muda wa wiki mbili.
Wajumbe wa baraza la kutunga katiba wakiidhinisha mswada huo
Katiba hiyo imechukua nafasi ya kati katika mzozo mbaya kabisa wa
kisiasa nchini humo tangu pale Morsi alipochaguliwa mwezi Juni mwaka
huu, ukiyahusisha kwa kiasi kikubwa makundi ya Kiislamu na wapinzani
kutoka makundi yenye misimamo ya wastani.
"Iilaaniwe bunge la katiba," kundi kubwa ambalo lilikuwa na vipaaza
sauti liliimba wakati wakiingia katika uwanja wa Tahrir, eneo
lililotumika katika vuguvugu ambalo liliuondoa madarakani hatimaye
utawala wa rais Hosni Mubarak mapema mwaka 2011.
Mabango yakimshutumu "Morsi kuwa ni dikteta" wakati waandamanaji
wakipaaza sauti "Ulaaniwe utawala wa kiongozi," wakiwa na maana ya
kiongozi wa chama cha udugu wa Kiislamu, ambapo Morsi alijitokeza
kupitia chama hicho kabla ya kuwa rais.
Rais wa Misri Mohammed Mursi
Maandamano msikitini
Maandanano mengine yalizuka wakati Morsi alipokuwa akisali katika
msikiti mjini Cairo, baada ya imam kuwataka Waislamu kumuunga mkono
rais, lakini hakukuwa na tukio kubwa.
Mapambano yalizuka katika mji wa kaskazini wa Alexandria baina ya
waandamanaji wanaomuunga mkono na rais Morsi na wale wanaompinga, duru
za usalama zimesema , lakini hakukupatikana taarifa mara moja za watu
waliojeruhiwa.
Maandamano yanatarajiwa kufanywa na kambi zote mjini
Cairo leo Jumamosi(01.12.2012).
Mzozo wa hivi sasa ulizuka baada ya rais Morsi kutoa tamko hapo Novemba
22 akijipa madaraka makubwa na kuwezesha uamuzi wake wowote kutopingwa
na mahakama, hali ambayo ilizusha maandamano pamoja na mgomo wa majaji.
Rais wa mahakama kuu ya katiba Maher Sami mjini Cairo
Katiba mpya huenda isipitishwe
Amri aliyotoa imezuwia chombo kikuu cha sheria , mahakama ya katiba kuwa
na uwezo wa kulivunja bunge linaloongozwa na kundi la Waislamu , katika
uamuzi ambao wangeuchukua siku ya Jumapili kuhusu uhalali wa kisheria
wa bunge hilo la katiba.
Bunge la katiba limeandika mswada wa katiba ambao utachukua nafasi ya
katiba ya zamani ambayo imesitishwa baada ya kuondolewa madarakani kwa
rais Hosni Mubarak mwaka jana , lakini kukamilishwa kwake kumesogezwa
mbele kutokana na mtafaruku uliosababishwa na amri aliyoitoa rais Morsi.
Maandamano yenye ghasia mjini Cairo.
0 comments:
Post a Comment