Aliyekuwa diwani wa viti Maalumu Chadema Mkoani Arusha, Rehema Mohammed,
akibubujikwa na machozi wakati akitangaza kujiunga na CCM, katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini
Arusha, juzi. UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umekunjua makucha na kuwapiga marufuku vigogo wanaowania urais kupitia chama hicho, kuwatumia kama ngazi ya kufanikisha malengo yao.
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Kaluta jana, Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis Juma
alisema kuna baadhi ya vigogo wenye malengo ya kuwania nafasi ya urais
wanawagawa vijana.
Mkutano huo ulihudhuriwa na vigogo wa chama hicho
akiwamo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Waziri Mkuu
aliyejiuzulu, Edward Lowassa na baadhi ya mawaziri.
UVCCM wamekuwa wakituhumiwa kutumiwa na vigogo walio katika mbio za kuwania urais mwaka 2015.
UVCCM wamekuwa wakituhumiwa kutumiwa na vigogo walio katika mbio za kuwania urais mwaka 2015.
Wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho,
imekuwa ikielezwa kuna wagombea urais waliokuwa wakihaha kuhakikisha
nafasi za uongozi wa jumuiya hiyo zinachukuliwa na vijana wanaowaunga
mkono.
Sadifa alisema makundi yaliyokuwapo kabla na baada ya uchaguzi wa jumuiya hiyo, sasa yanatakiwa kuvunjwa na kujenga umoja huo kwa masilahi ya chama.
Sadifa alisema makundi yaliyokuwapo kabla na baada ya uchaguzi wa jumuiya hiyo, sasa yanatakiwa kuvunjwa na kujenga umoja huo kwa masilahi ya chama.
Alisema kitendo cha wanaotaka urais kuwatumia vijana kama ngazi, sasa watambue kuwa hawapo tayari kwa hilo.
“Ni wakati mwafaka kuwaambia hao wanaotaka urais, sisi siyo ngazi ya kupandia,” alisema.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo ya wananchi.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo ya wananchi.
Nape alisema safu mpya ya CCM imekuwa tishio kwa
upinzani na kuongeza kuwa, kimejipanga vyema. “Sifa ya Katibu Mkuu wa
CCM, Kinana, huwezi kufananisha na Katibu Mkuu wa chama chochote cha
siasa nchini.
Pia, safu yetu nayo imekamilika kila kona ndiyo maana wapinzani wanapata tabu na wanahangaika kuzima moto wetu lakini wanashindwa,” alisema Nape.
Kinana kurudisha imani
Mbinu iliyotumiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na sekretarieti yake kukiri makosa yaliyofanywa na chama hicho na kutaka kurejesha utaratibu wa kukosoana, ndiyo sababu baadhi ya wanachama wameanza kurejesha imani.
Pia, kusudio la kutaka kuvirejesha viwanda vya kubangua korosho vilivyonunuliwa na wafanyabiashara, ni sehemu ya mambo yaliyowavutia wanachama.

Jana, Kinana alimaliza ziara yake mikoa ya Mtwara,
Rukwa, Geita na Arusha kwa kusema kuwa, wananchi walianza kukichukia
chama hicho kwa sababu viongozi wake walikuwa hawatatui matatizo yao.
“ Ni lazima tukubali kuwa chama kilifanya makosa ambayo yanahitaji kurekebishwa.
Pia, wanachama wanatakiwa kuwakosoa viongozi wao wanapokosea ili kukabiliana na changamoto zilizopo,” alisema Kinana.
“ Ni lazima tukubali kuwa chama kilifanya makosa ambayo yanahitaji kurekebishwa.
Pia, wanachama wanatakiwa kuwakosoa viongozi wao wanapokosea ili kukabiliana na changamoto zilizopo,” alisema Kinana.
Kinana alisema viongozi waache kuitwa waheshimiwa hilo ndilo linalowafanya wawe mbali na wananchi.
“Viongozi wa chama wanatakiwa kuwa watumishi na kuachana na uheshimiwa,” alisema Kinana.
Wakati akianza ziara yake mkoani Mtwara, wananchi hawakuwa na furaha, lakini alipotangaza kusudio la kuibana serikali kuwanyang’anya vigogo wasiondeleza viwanda vya korosho, wananchi walifurahi huku matarajio yao yakiwa kupata ajira.

0 comments:
Post a Comment