
WAASI wa Syria wamesema leo (19.11.2012) kwamba wameiteka kambi kubwa ya
jeshi kwenye barabara kuu kati ya mji wa Aleppo na mpaka na Uturuki.
Shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limetoa mkanda wa
video unaoonyesha waasi wakiwa ndani ya kambi ya Orum al-Sughra katikati
ya vifaru na silaha walizokuwa wameziteka.
Kwa mujibu wa wanaharakati
wa upinzani, wanajeshi wasiopungua 25 walio watiifu kwa rais wa Syria,
Bashar al Assad, wamechukuliwa kama wafungwa wa kivita.
Taarifa ya shirika la habari la Aleppo imesema vifaru takriban 15
vimetekwa.
Mwanaharakati wa upinzani katika eneo la kaskazini la Syria,
Mohammad Abdallah, amesema silaha zilizokuwa katika kambi hiyo zilikuwa
zikitumiwa kufanyia mashambulizi ya mabomu katika miji na vijiji katika
viunga vya mji wa Aleppo na mkoa jirani wa Idlib.
Kambi hiyo inapatikana
kilometa 25 magharibi mwa Aleppo, kati ya mji huo na mpaka na Uturuki.
Upinzani wa Syria umetuma pia mkanda wa video ukionyesha mapambano
makali karibu na kambi ya jeshi ya Nairab mjini Aleppo, mkoa wa
mashariki wa Deir al Zour na maeneo ya viunga vya mji wa Damascus.
Uholanzi na Ujerumani kuisaidia Syria
Wakati huo huo, Uholanzi na Ujerumani zinatafakari kuipelekea Uturuki
makombora kuisaidia kuulinda mpaka wake na Syria.
Uturuki imesema
imefanya mazungumzo na washirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO kuhusu
njia ya kuimarisha usalama katika mpaka wake wa kilometa 900 na Syria
baada ya makombora kuanguka katika himaya yake kutoka Syria.
Waziri wa ulinzi wa Uholanzi, Jeanine Hennis-Plasschaert, amesema
jumuiya ya NATO haipo kufanya kazi bure.
Shirika la habari la ANP nchini
Uholanzi limemnukulu waziri huyo akisema Uturuki haijawasilisha ombi
rasmi lakini Uholanzi na Ujerumani ndizo nchi zenye wazalendo barani
Ulaya.
Shirika la ANP limesema waziri Jeanine alijadiliana na mwenzake
wa Ujerumani wiki iliyopita kuhusu uwezekano wa kuisaidia Uturuki.
Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kuijadili Syria
Hii leo mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini
Brussels kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu masuala tete katika eneo la
Mashariki ya Kati, lakini vile vile kutofuata mkondo wa Ufaransa
kuutambua rasmi upinzani mpya wa Syria.
Umoja huo kwa muda mrefu umetoa
mwito vuguvugu la upinzani liungane kumuondoa madarakani rais wa Syria,
Bashar al Assad.
Bashar al-Assad.
Kwenye ujumbe wake wa leo makundi makubwa ya waasi wa kiislamu mkoani
Allepo, yakiwemo Al-Nusra Front na Liwa al-Tawhid, yameukataa muungano
mpya wa upinzani, yakisema yanataka taifa la kiislamu.
Urusi yalaumiwa
Kwa upande mwingine Canada imeinyoshea kidole cha lawama Urusi kwa
kutofanya lolote kuisaida Syria huku nchi hiyo ikitumbukia katika
matatizo mazito.
Waziri wa ulinzi wa Canada, Peter McKay amesema
mwishoni mwa mkutano wa kimataifa wa usalama uliofanyika jana huko
Halifax kwamba Urusi inalazimika kufanya mengi zaidi.

0 comments:
Post a Comment