Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri Mohamed Morsi wameitisha maandamano makubwa leo Ijumaa baada ya kiongozi huyo kujipa madaraka makubwa ambayo wachambuzi wansema kuwa yanamfanya kuwa dikteta.
Safu ya vikundi huria na visivyo na mlengo, ikiwa ni pamoja na
wanaharakati waliokuwa mstari wa mbele katika harakati zilizomwondosha
madarakani kiongozi mkongwe wa taifa hilo.
Hosni Mubarak mapema mwaka
jana, wamepanga kufanya maandamano katika bustani ya Tahrir jijini
Cairo, eneo ambalo ni kitovu cha maandamano, kupinga hatua ya kiongozi
huyo ambaye amebatizwa jina la farao mpya.
Wafuasi wa Morsi wakiongozwa na chama chenye nguvu cha Muslim
Brotherhood wamekusanyika nje ya kasri ya rais Kaskazini mwa jiji la
Cairo kuonesha kuunga mkono uamuzi wa rais huyo kujiongezea madaraka na
kujiweka juu ya sheria za nchi hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa rais Morsi anatafakari kuhusu kuhutubia umma
wa taifa la Misri baadye hii leo kwa lengo la kutetea uamuzi wake.
Siku ya Alhamisi, rais alidhoofisha uwezo wa mahakama ambayo imekuwa ikifikiria kuweka usawa katika jopo linalotawaliwa na chama hicho cha kiislam kwa kutengeneza katiba mpya, kwa kuwaondolea majaji haki na mamlaka ya kuhoji kuhusu maamuzi yake.

0 comments:
Post a Comment