JE unafahamu kuwa Wanawake wana uwezo mkubwa zaidi wa kunusa.
Wenyewe hawajui lakini, mwamke anaweza kunusa
hasira, naam ikiwe mumewe ana hasira hata akikaa kimya , mkewe atakuwa
wa kwanza kujua kwamba mmmh !
leo kumeharibika.
Mwanamke pia anaweza kunusa uongo wa mumewe.
Dr Gün Semin wa Utrecht University, Ujerumani anasema hii ni kutokana na jasho la mwanamume !.

Utafiti unaonyesha kuwa jasho analotoka
mwanamume linatuma ujumbe katika kiwili wili cha mwanamke na
kumuambukiza hali unayosikia bila ya wewe kumuambia kitu.
Jasho lako
linatuma ujumbe kwa mkeo au kwa mchumba wako.
Ukiwa wewe mwanamume umeshutshwa na kitu au
umebabaika au umeogopa au ana hasira. Jasho lako litasema.
Na System ya
mama itapokea ujumbe !.
Dr Gün Semin wa Ujerumani anasema mwanamume
akikasiria anatoa jasho lenye kemikali aina fulani.
Akiwa na uoga
anatokwa na jasho aina tofauti.
Ndio maana mkeo au mchumba wako atakuuliza kuna
nini lakini ?.
Hata ukikataa mwili wake unamuashiria kwamba lazima kuna
kitu.
Sio ati wao ni wajanja sana lakini jasho lako limetoa chembechembe
fulani kulinagani na hali yao na hivyo kutuma ujumbe wa siri kwa system
ya mama.
Ni majaliwa ya wanawake hayo.

Kipepeo aweza kunusa mpenzi wake akiwa mbali
Vipepeo wanawake pia wanamajaliwa ya kuweza kunusa vitu.
Wanasayasi wanasema kipepeo ana uwezo wa kunusu kipepeo mchumba wake au anayemfaa hata akiwa maili 7 au nani hivi.
Kipepeo atanusa nakujua kiboko yangu anakuja japo yuko kilomita nyingi.
Nani mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kunusa? Kwa wanyama ni Dubu, yaani bear, sio teddy bear.
Baharini ni papa. Papa anaweza kunusa hata damu amboyo bado ingali ndani ya samaki mwengine.
Ni papa huyo.

0 comments:
Post a Comment