WANANCHI wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam,wamesema kuwa katiba itakayopatikana iruhusu siku ya ijumaa iwe siku ya mapumziko.
Wakitoa
maoni yao kwa nyakati tofauti mbele viongozi wa Tume ya Kukusanya
Maoni, walisema kwamba siku hiyo iwe rasmi ya mapumziko kwa kuwa waumini
wa dini ya kiislamu wanatakiwa wawe kwenye ibada na siyo kazini.
Mkazi
wa Kata ya Jangwani,Rashidi Musa alisema katiba ikiruhusu siku hiyo
iwe siku ya mapumziko itatoa fursa kwa waumini wa dini hiyo kwenda
kwenye ibada kwa wakati.
Musa alisema watu wanapokuwa kazini
wanabanwa na kazi hivyo wanashindwa kwenda kwenye ibada matokeo yake
kila ikifika siku hiyo anakosa nafasi.
“Ile siku iheshimiwe iwe
kama siku ya Jumamosi na Jumapili kwa nini siku hii ikifika watu wengine
wanafanya kazi nusu siku na wengine wanafanya kazi siku nzima ambapo
wanakosa muda wa kwenda kwenye ibada ya Ijumaa”alisema Musa.
Naye
Mkazi wa Kata ya Gongolamboto, Gaudensia Busta alisema katiba
itakayoundwa iseme kuwa wafungwa wanaotumikia vifungo wawe wazalishaji
wakuu wanapokuwa magerezani.
Alisema utakuta wafungwa
wanarundikana magerezani wakati serikali ilitakiwa kuwatumia hao katika
uzalishaji kama kulima mazao mbalimbali kwa ajili ya chakula kiweze
kupelekwa hospitalini na magerezani.
“Kama Serikali itawatumia
wafungwa watumike kama wazalishaji wakuu wanapokuwa magerezani, nina
imani wataweza kulima mazao mbalimbali na kupelekwa hospitalini ili
chakula hiki kiwasaidie wagonjwa ambao hawana ndugu”alisema Busta
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment