BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFANYABIASHARA WA MAGENDO WAIZIDI SERIKALI

WAKATI Kenya ikiwa imezuia malori yaliyosheheni sukari kutoka Kiwanda cha TPC yaliyokuwa yakisafirisha sukari kihalali , sukari inayosafirishwa kimagendo imeendelea kuvuka mpaka kila siku kwenda nchini humo kupitia maeneo ya mpakani ya Mkoa Kilimanjaro.

Taarifa za uhakika zilizopatikana jana mjini Moshi, zilisema licha ya doria ya polisi na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), maeneo ya Himo, Holili na Njiapanda bado juzi alfajiri malori mawili yalivuka mpaka kwenda Kenya yakiwa na sukari.

Malori hayo yanadaiwa kuvuka mpaka kupitia eneo la Kileo hadi Mnoa wilayani Mwanga na baadaye kuingia eneo la Madarasani nchini Kenya, njia ambayo ni maarufu kwa biashara ya magendo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Jaffar Ally anayeshughulikia utawala alisema ingawa Serikali iliwapa kibali cha kusafirisha tani 5,000 kwenda nje ya nchi, lakini sukari hiyo imekwama upande wa Kenya kutokana na urasimu mkubwa.

Ally alisema baada ya kutolewa kwa kibali, wafanyabiashara waliopewa kibali walipakia shehena katika malori matatu na kuelekea Kenya kupitia Namanga lakini wamekwama kwa wiki tatu kutokana na urasimu wa Serikali ya Kenya.


“Tunaambiwa Namanga upande wa Kenya wanawataka hao wafanyabiashara waweke dhamana ya asilimia 100 yaani kama shehena yako ina thamani ya Sh1 bilioni basi uweke dhamana ya kiasi hicho”alisema Ally.

Ofisa huyo alionyesha kushangazwa kwake na urasimu huo na kuhoji” Sukari inayokwenda kihalali Kenya wanawekewa vizingiti, lakini sukari ya magendo inadaiwa kuvuka mpaka kila siku.

Ofisa huyo alisema mauzo ya sukari katika kiwanda hicho yamefikia tani 400 kwa siku na kuonyesha wasiwasi wake juu ya kuwapo kwa soko kubwa na la ghafla la sukari mjini Moshi.


Wakati kukiwa na soko hilo la ghafla, taarifa nyingine zinadai sukari kutoka Kiwanda cha Kilombero ambayo inauzwa na kiwanda hicho kwa kati ya Sh74,000 na Sh75,000 inaingizwa mkoani Kilimanjaro.


Chanzo kimoja kutoka taasisi nyeti kimelidokeza gazeti hili kuwa, ni lazima ipo agenda ya siri kwani gharama za kusafirisha sukari hiyo kuja Moshi ni kubwa kulinganisha na ile ya Sh76,000 ya TPC.

“Tunajiuliza kama TPC wenyewe wanauza tani 400 kwa siku na hapo hapo Sukari kutoka Kilombero nayo inaingia Kilimanjaro inakwenda wapi…ni Sukari nyingi sana”kilihoji chanzo hicho.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: